AMANI IDUMISHWE

 Amani ni hali ya kutokuwa vita katikati ya nchi kwa sababu vita huleta uharibifu mkubwa kushinda aina nyingine za ugomvi.

Je, Ni njia gani zinafaa kutumika Ili kudumisha amani ?

Serikali kupambana na ugaidi nchini Kenya. Serikali inafaa kuweka sheria maalum za kupambana na ugaidi kote ulimwenguni. Hizi sheria ni pamoja na zile zinazohusu utekaji watu nyara,mlipuko wa mabomu inayosababishwa na magaidi.

Kukuza uhuru wa magazeti na ule wa kujielezea Ili kuwaruhusu watu wote waweze kutoa habari ambazo hazitakaguliwa na kutokuwa na ubaguzi wa kitamaduni,ni dhahiri shairi kuwa,serikali imesaidia kustawisha na kuimarisha vyombo vya habari.

Serikali kubadilisha mitaa ya mabanda iwe makao yafaayo kwa binadamu.Miji mikuu imekuwa makao kwa nusu ya watu ulimwenguni.wamekuwa kitovu Cha shughuli za uzalishaji Mali na kutumia.Pia hushughulikia namna za kutega uchumi na uimarishaji wa jamii Ili kupata Mali na nafsi bora.Pia serikali inafaa kutoa usalama wa umilikaji kwa wale wakazi maskini wa mjini, jambo Ili litakuwa kama kichocheo Cha rasilimali kwa huduma za kimsingi na nyumba kwa watu maskini.

Kulinda rasilimali za wasomi.Shirika la Mali ya wasomi ulimwenguni linafaa kulinda haki za wasanii na wanaomiliki rasilimali za wasomi kote ulimwenguni na kuona kwamba wavumbuzi na waandishi wanajulikana na kupewa tuzo kwa ubunifu wao.

Tunatakiwa tushirikiane kwa ujenzi wa Kenya hii yetu Ili kulinda amani na kusonga mbele hata kiuchumi.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

CHILD LABOR

TOXIC RELATIONSHIP AMONG CAMPUS STUDENTS

UMASKINI SI KIFO