UMASKINI SI KIFO

 Hakika,omba omba anajua bahili. Mnamo mwaka wa 2012, januari shida zilitukumba kifamilia na kutuwangaisha .

Hii ilitokea punde tu Babu yangu alipoaga dunia.Sitasahau asilani, nilikuwa darasani mida ya saa  sita mchana ndipo mwalimu mkuu aliingia na kuniita kwa jina langu "Sami, njoooooooooo!" Kisha akaondoka.

Punde si punde niliandamana naye Hadi ofisini mwake bali nilikuwa nawaza na kuwazua alichonitia huku jakamoyo zikinijaa. Mwalimu mkuu aliniambia," naomba ukauchukue mkoba wako moja kwa moja uwasili nyumbani ". Ni dhahiri shairi fikra zilinizidi na maswali mpururo yalinijaa.

Njiani,nilikuwa natembea aste aste huku nikiwaza ni nini haswa nilichomfanyia mwalimu mkuu ,hata hivyo mwili wangu ulizidi kulegea.

Nilipokaribia kwa lango la boma yetu,niliona adnasi wengi wameketi huku wamejawa na huzuni  ilhali nyanya yangu alikuwa anatiririkwa na machozi. Nilijikakamua hadi sebuleni mwetu na kupata wazazi wangu kama wameketi kitako lakini hamna aliyezungumza  na mwengine.


Baada ya dakika chache,jirani Tende aliingia sebuleni na kusema," jitieni moyo , Mola hakosi !Babu alale salama". Baba yangu akadakia,"Baba yangu hayupo tena."Nilipiga nduru iliyofanya viziwi wasikie .


Nilipiga taswira jinsi Babu yangu alivyougua kwa muda mrefu huku tukitarajia kupona kwake lakini ikawa kinaya. Mambo yalianza kwenda mrama kwa sababu deni ilikuwa  milioni moja ambapo ilitugharimu  wa familia kuilipa. 

Baada ya kikao Cha familia,walisuluhisha kuuza Mali waliorithi ili kulipa deni la hospitali.

Baada ya Mazishi ya babu yangu tulibaki maskini hoe hae kwani senti haikuweza kupatikana katika boma yetu. Wazazi wangu walitia bidii Ili tujikimu kimaisha lakini haikuwezekana. Ilibidi niwache shule nikajitafutie pamoja na familia yetu nikijua kwamba , mwombaji ana milango mingi.

Mwishowe , baba yangu alipata ajira Nairobi ambapo ilitugharimu kila kitu.

Yamkini,baada ya dhiki ni faraja.





Comments

  1. πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜’πŸ˜’......

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

CHILD LABOR

TOXIC RELATIONSHIP AMONG CAMPUS STUDENTS